Kenya yaandaa magari kadhaa kwa mapambo ya michoro kumkaribisha Mfalme Charles III

Magari hayo manne yaliyopambwa kwa grafiti yalionyeshwa katika kituo cha Greenpark jijini Nairobi.

Muhtasari

• Matatu hizo nne zilizopambwa kwa grafiti zlionyeshwa katika kituo cha Greenpark jijini Nairobi

• Mfalme Charles III na Malkia Camilla watazuru Kenya kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 3, 2023 kwa ziara rasmi.

 Ubalozi wa Uingereza nchini Kenya Ijumaa ulizindua matatu za kifalme kabla ya ziara ya Mfalme Charles III na Malkia  Camilla nchini wiki ijayo.

Magari hayo manne yaliyopambwa kwa grafiti yalionyeshwa katika kituo cha Greenpark jijini Nairobi.

Matatu hizo  zimepambwa kwa bendera ya Uingereza iliyochapishwa mbele, pamoja na ile ya Kenya.

Kwenye pande ya Matatu, Masaai Moran akiwa amebeba bendera ya Uingereza, na mguso wa picha ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenya kuashiria Nairobi CBD, pamoja na twiga, na Pundamilia pembeni kwa mbuga za Kitaifa zinazozunguka nchi.

Katika graffiti, Morans wa  kimasai wamevaa mavazi yao ya kitamaduni, zingine zimepambwa kwa picha ya wachezaji wa Kenya Sevens, flamingo wa Nakuru, na mwanariadha wa Marathoni Eliud Kipchoge.

Zaidi ya hayo, matatu nyingine zina picha za Wakuu hao  Mfalme Charles III na mkewe, Malkia Camilla.

Mapambo hayo yalifanywa na Msanii maarufu wa Graffiti Graff Matwana, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Matwana Culture.

Wakuu ha watakapotua nchini Kenya, matatu za kifalme zilizopambwa zitakuwa sehemu ya msafara wao na zitasafirisha baadhi ya maafisa, kutoka kwa ubalozi.

Mfalme Charles III na Malkia Camilla watazuru Kenya kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 3, 2023 kwa ziara rasmi.

Hii itakuwa ni ziara ya kwanza rasmi ya Charles nchini Kenya tangu kutawazwa kuwa Mfalme mnamo Mei 2023, na ya kihistoria kwani hii ndio nchi ambayo mama yake alitangazwa kuwa Malkia Elizabeth II, baada ya kukalia kiti cha ufalme nchini Kenya mnamo Februari 1952.

Malkia Elizabeth II alikuwa na umri wa miaka 25 wakati huo.

Katika ziara yao, Mfalme na Malkia watakutana na Rais William Ruto na Mke wa Rais Mama Rachel Ruto, pamoja na wajumbe wengine wa serikali, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Mfalme pia atahudhuria hafla ya kusherehekea maisha na kazi ya Mshindi wa Tuzo ya Nobel marehemu Profesa Wangari Maathai, pamoja na bintiye Wangari, Wanjira Mathai.