Hatari kwa taifa! Wizara ya afya yawatafuta watu 140 waliopatikana na virusi vya corona

Serikali sasa imeanzisha mchakato wa kuwatafuta watu 140 waliopatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo katika maeneo tofauti yaliyokuwa yametengwa nchini na wizara ya afya .

Kupitia kwa mkurugenzi mkuu wa afya nchini Dr Patrick Amoth,wakenya hao walipatia taarifa za uongo wakati ambapo walikuwa wanafanyiwa vipomo hivyo na baada ya matokea yao kutoka ,imekuwa vigumu kwa serikali kuwapata waliko.

“As the CS said, they can run but cannot hide from the long arm of the government. They can choose to present themselves before the disease puts them down,” amesema Amoth.

Taarifa ya Amoth inajiri siku chache tu baada ya kubainika kuwa mgonjwa mmoja alitoroka katika hospitali ya Mbagathi baada ya kuwatishia madaktari na hata bawabu.

Kufikia sasa Kenya imesajili visa 1745 apo wagonjwa walioko nchini ama active vcases katika kaunti zote 37 zilizoathirika ni 671.

Kulingana na Amoth baadhi ya wakenya 130 wametengwa katika nyumba huku watu kutoka mataifa ya kigeni 30 wakirudishwa makwao baada ya kupatikana na virusi hivyo.