Ibada ya kumbukumbu ya mwanaharakati Caroline Mwatha

Caroline-Mwatha
Caroline-Mwatha
Ni kifo ambacho mwendazake mwanaharakati Mwatha aliweza kukumbana nacho, mwanaharakati huyo aliweza kuuwawa kwa hali tatanishi.

Daktari wa upasuaji aliweza kusema kuwa Caroline aliweza kuaga dunia kwa sababu ya kuavya mimba, matukio ambayo wanaharakati na familia waliweza kupinga kwa ukali mwingi.

Ibada ya kumbukumbu iliweza kufanyika katika eneo la Uhuru Park Freedom corner Alhamisi.

Jana mwanaharakati Kegoro aliweza kusema kuwa Caroline aliweza kuuwawa na wala si kuavya mimba.

Mwatha 37, atazikwa nyumbani kwake Rarieda katika kaunti ya Siaya Ijumaa, 22, ibada hiyo ili weza kutayarishwa na watetezi wa haki za binadamu.

Walioudhuria ibada hiyo ni pamoja na aliye kuwa jaji mkuu wa mahakama ya juu Willy Mutunga, mwanasiasa Martha Karua na Esther Passaris na pia mtendaji wa tume ya utetezi wa haki George Kegoro.

Baba yake mzazi wa mwendazake mwanaharakati huyo Stanislaus Mbai alikataa madai ya kuwa mwanawe Caroline hakufariki kwa kuvuja damu baada ya kuavya mimba.

" Sitawahi elewa mbona sikugundua uja uzito wa Caroline, kwa maana hakukua na dalili yeyote katika picha ambazo marafiki zake waliweza kueka katika mitandao wiki ambayo mwanangu aliweza kupotea, " Mbai alizungumza.

Aliweza kuomba wananchi waombee familia hiyo, huku ibada hiyo ikitendeka mume wake mwanaharakati huyo Joshua Ochieng hakuwa na nguvu yeyote ya kuongea ata mama mkwe wa Caroline.

Katika ibada hiyo mwanaharakati hakuweza kunyamaza bali alisema kuwa Caroline aliweza kuuliwa na hatokubaliana na matokeo ya upasuaji.

" Mwatha alifanya kuuwawa, hata kama uchunguzi unaendelea kufanyika, tunajua ukweli kuwa Mwatha hakujiua,

" Tunajua kuwa aliweza kuuwawa na mtu ambaye hakupendezwa na kazi ya Mwatha, " Alisimulia Kerogo.

Pia aliyekuwa jaji mkuu Willy aliweza kusema katika ibada hiyo kuwa hakuweza kuamini ripoti hiyo ambayo ilipeanwa na polisi hao.

Nani atakaye tetea haki ya mwanaharakati huyo kama alivyotetea haki za wananchi eneo la Dandora kaunti ya Nairobi.

Mwanaharakati mkongwe Timothy Njoya alisema kuwa Caroline aliishi mwaisha ya ukombozi pia aliweza kuongezea na kusema kuwa wanasherehekea maisha ya marehemu.

Pia marafiki na familia waliudhuria ibada hiyo ambayo ilianza saa nane mchana.