Ilikuaje:Siwafahamu wazazi wangu tangu utotoni mwangu-Leila Chepkirui

IMG_5013
IMG_5013
Leo katika kitengo cha ilikuaje Leila Chepkirui alieleza jinsi alivyolelewa na watu tofauti huku akihishi mtaani kwa kukosa wazazi wake na jinsi mwanawe alijiunga na kundi la Alshabaab.
"Hadi sasa sijui wazazi wangu halali, hii ni kwa sababu wazazi wangu walikuwa wnataka kuniavya lakini yaya ambaye alikuwa ameandikwa kwetu alimkataza mama yangu

Alimwambia anizae na ampe mtoto, sijui kwanini au makubaliano waliokuwa nayo wakati huo, baada ya hapo nyanya huyo alinichukua na kuanza kunilea

Baada ya muda nyanya aliaga dunia na kuachwa katika chumba cha watoto mayatima, ilifika muda tukaambiwa hatupaswi kuwa katika eneo hilo

Wale wengine walikuwa wanalelewa nami walichukuliwa nami nikaachwa nilienda kuishi mitaani." Alisimulia Leila.

Alizidi na kuzungumza,

"Kwa sababu sikuwa na chakula mwanaume mmoja alichukua fursa ya kunitumia ili nipate chakula hapo ndipo nilipata ujauzito

Nilijifungua mtoto wa kiume, kwa niliishi mitaani na yeye nilikuwa nasaidiwa na  watu kutoko msikitini na kanisani, watu walichukua nafasi hiyo kumhuzisha katika vitendo mbalimbali

Msikiti uliamua kumsomesha mtoto wangu kwa maana sikuwa na uwezo, kuna mwalimu ambaye alikuwa anajiita wa dini ambapo nilimkubali kijana wangu kujiunga

Lakini hayakuwa masomo ya dini mbali walikuwa wanafunzwa jinsi ya kuwa gaidi, katika kidato cha pili alibadilika ghafla na kuacha masomo

Hii ni kwa sababu nilikuwa nakula miraa, na hata kulewa watoto wangu wakiwa hapo, nilibarikiwa na mtoto mwingine msichana ambaye alikuwa anachapwa sana na ndugu yake baada ya kubadilika

Nilimuongelesha lakini siku moja aliamka na kuniambia anataka kuenda Somalia." Leila Alisimulia.

Baada ya kijana wake kubadilika Leila alienda kupata msaada kutoka kwa chifu ili kijana wake hasiweze kujiunga na kundi la Alshabaab.

Ilimbidi aende mpaka kwa serikali ili mwanawe abadilike, kijana huyo alifuatiliwa na serikali na mwishowe kubadilika.

"Baada ya kufuatiliwa nilimrudisha shule na kisha akamaliza shule ya upili, na nilimuokoa kwa sasa amebadilika na anaendelea vyema

Nimewalea watoto wangu pekee kati ya vijana ambao waliokuwa na wao yeye tu ndio amesalia na kubadilika." Alisema.

Kwa mengi zaidi tembelea mtandao wetu wa kijamii wa youtube.