ILIKUAJE:Ilichukuwa miaka mitano ili wimbo wangu wa kwanza uwe maarufu-Gloria Muliro

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa na mgeni ambaye ni muimbaji wa nyimbo za injili Gloria muliro, akielezea safari yake ya uimbaji.

Hivi majuzi Gloria  ameutoa wimbo ambao unajulikana kama 'Look to Jesus' na kusema kuwa aliimba wimbo huu kwa ajili ya kuwatia watu ambao wamepitia changamoto na kukufa moyo.

"Huo wimbo niliimba kwa ajili ya kuwatia watu moyo ambao wanapitia changamoto nyingi sana." Alisema.

Aliendelea na kusema kuwa alipoanza kuimba ilimchukua muda wa miaka mitano ili ajulikane na nyimbo zake zij++++++++++ulikane.

"Niling'ang'ana sana kwa kutoa wimbo wangu wa kwanza ambapo ilichukua muda wa miaka mitano ili wimbo wangu ujulikane,

Wimbo wangu uliopokolewa sana na kupendwa sana ni wa 'omwami' wimbo ambao ulipokelewa sana na watu wa nyumbani

Hii ni baada ya kuenda nyumbani na kuenda kuimba nyumbani kwetu." Alizungumza Gloria.

Gloria alizidi na kueleza changamoto alizozipitia baada ya mama yake kuaga dunia na baba yake kuoa mama wa kambo.

"Baada ya mama yangu kuaga dunia baba alioa mama wa kambo, na tuka pitia shida na changamoto nyingi sana, 

Kabla ya kuwa muimbaji nilikuwa mwalimu, na kwa sababu ya wito wa Mungu niliacha kazi hiyo na kuanza kuimba." Gloria Alisema.

Akiongelelea kuhusu kifo cha msanii mwenda zake Papa Dennis alikuwa na haya ya kusema,

"Kwa hakika hadi waleo hakijawahi bainiwa kiini cha kifo cha Papa, Mila ndiye anajua yote na yale yalitendeka." Alizungumza.

Msanii Gloria alikuwa katika mstari wa kwanza katika kupanga mazishi ya Papa na hata akaenda na kuhudhuria mazishi yake licha ya wasanii wengi kutojitokeza siku hiyo.