Jaguar alikuwa mshauri wangu, Vivian asema

Wengi walifikiri wawili hao walikuwa na uhusianao miaka mitano iliyopita, lakini Jaguar alikuwa mshauri wake tu na kuhakikisha kuwa jina lake lilijulikana katika sekta ya burudani, Vivian alisema kwenye mtandao wa Instagram.

 
"Huyu ni mimi pamoja na Mheshimiwa Charles Njagua kama wengi wenu mnavyomjua. Picha hii ilichukuliwa miaka mitano iliyopita." Vivian alisema.

"Alikuwa zaidi ya Jaguar wakati huyo, na alikuwa amekuja kuniunga mkono ma wakati huo Philip Makanda aliyekuwa mzalishaji wangu aliichukua picha hii.

Kulikuwa na uvumi mwingi sana kwamba tulikuwa na uhusiano miaka mitano iliyopita jambo ambalo halikuwa la kweli.

Vivian, ambaye sasa yu Marekani, alisema alizungumza na Jaguar na kusema afadhali angekuwepo.

Soma mengi