Jaribio la mapinduzi: Maafisa wakuu wa kijeshi wakamatwa Sudan

AFPCopyright: AFP Gen Mohamed Othman al-Hussein announced the arrests
AFPCopyright: AFP Gen Mohamed Othman al-Hussein announced the arrests
Jeshi nchini Sudan limetangaza kwamba baada ya kutibuka kwa jaribio la kupindua serikali maafisa kadhaa wa vyeo vya juu na wanachama wa kilichokuwa chama tawala National Congress Party (NCP) wamekamatwa.

Bado haijabainika ni lini jaribio hilo la mapinduzi lilifanyika, lakini huenda mamlaka nchini humo inazungmzia jaribio linalodaiwa kufanyika mapema mwezi huu.

Habari zaidi:

                         :

Habari hizi zinajiri wakati majenerali wa kijeshi wanaoongoza serikali na vunguvu la upinzani wanapotarajiwa kuendelea na mazungumzo ya kukamilisha makubaliano ya ugavi wa mamlaka nchini humo. Waliokamatwa wanajumuisha aliyekuwa mkuu wa majeshi, Jenerali Hashim Abdel Mottalib Ahmed na mkuu wa kitengo cha kujihami, Meja Jenerali Nasr Ali-Din.

Wengine waliokamatwa ni aliyekuwa makamu wa rais Bakri Hassan Salit na aliyekuwa waziri wa mashauri ya kigeni katika serikali iliyong’olewa mamlakani ya Rais Omar Al-Bashir. Taarifa ya kijeshili ilisema kwamba jaribio hilo la mapinduzi lililenga kurejesha mamlaka kwa chama NCP chake al-Bashir.

Mkuu mpya wa majeshi, Generali Mohamed Othman al-Hussein alisema:

“jaribio la mapinduzi lililotibuka lilikuwa na nia ya kuvuruga mipango ya kuleta uiano wa kisiasa kwa lengo la kurejesha utawala wa kiraia unaongwa mkono na wananchi wengi nchini Sudan”.