Jinsi mwanamke alivyohadaa na kuvuna Mamilioni kwa kutumia majina ya Rais Uhuru, Ruto

Ni mshangao mkubwa sana kushuhudia  jinsi ulaghai  unavyoendeshwa hususan kwa kutumia  majina ya watu mashuhuri na idara muhimu za serikali zinazojulikana hadharani.

Mwanamke mmoja aliyedai kuwa mfanyakazi wa Ikulu ameshangaza watu wengi kwa kupata mkataba na  zabuni ya kandarasi ya vifaa vya kiuchunguzi vya kijeshi, vifaa vya kiufundi.

Na katika kisa kingine alijidai kuwa mfanyakazi katika afisi ya naibu wa rais William Ruto na akapewa zabuni yenye kima cha shilingi milioni 180 ambapo alitarajiwa kusambaza vipatakilishi 180 aina ya HP.

Katika kesi hizo mbili, walalamikaji walimshtumu Wangari Kamua ambaye anajulikana kwa jina la msimbo kama Patricia Mareka.

Kulingana na mwendesha mashataka na mashahidi, Kamau anatumia majina bandia na kujifanya kuwa meneja kwatika afisi za kutoa zabuni na kandarasi katika Ikulu au jumba la Harambee.

Na wakati mwingine, Kamau alijidai kuwa  miongoni mwa maafisa wa ujasusi wa jeshi.

Mnamo Jumanne mwanamke huyu ambaye amekuwa akisakwa kwa mwaka moja sasa alisimama kizimbani mbele ya hakimu mkaazi wa  mahakama ya Kiambu.

Alishatkiwa kwa makosa mengi ya kughushi zabuni pamoja katika idara ya ulinzi na Ikulu.

 

Hakimu mkaazi mwandamizi wa Kiambu Stellah Atambo alimwamuru Kamau kusalia rumande katika gereza la wanawake la Lang'ata. hadi Novemba 5.

Mwanamke huyu anashtumiwa kwa kumlaghai Charles Ng’ang’a shilingi milioni 40 na  mlioni 96 nyingine kwa kudai kuwa angempa zabuni ya kusambaza  vifaa vya kiuchunguzi ikiwemo vipatakilishi 10 aina ya HP yenye thamani ya shilingi milioni 96.

Kamua alishatakiwa kwa madai ya ulghai pamoja na udanganyifu  kwa kujidai kuwa afisa wa serikali anayehudumu katika Ikulu.

Wakili wake Njau Kayai alirai hakimu kumwachilia kwa dhamana akidai kwamba mteja ana akili taira na hangetoroka akipewa dhamana.

Hata hivyo maombi hayo yalikataliwa na mwendesha mashtaka akisema kwamba mshukiwa alihepa kesi alipoachiliwa kwa dhamana kutoka kwa kesi nyingine kama hiyo ya ulaghai.

Kayai aliambia korti kamba mteja wake hakuwa ameonekana kortini kwa kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili na hangeelewa sheria za dhamana aliyopoewa.