JUJA: Waumini Wamfurusha Mchungaji Mpenda Pesa

preacher-black-and-white-silhouette-600x410
preacher-black-and-white-silhouette-600x410
Leo ikiwa Jumatatu, kama ibada kipindi ukipendacho cha Gidi na Ghost Asubuhi kilirudi hewani baada ya wikendi refu na kama kawaida Ghost Mulee alirudi na uhondo kamili kutoka majimbo tofauti.

Tukizungumzia ibada, kulikuwa na vituko maeneo ya Juja katika kanisa moja hapo jana.

Kulingana na Ghost Mulee, waumini walimtimua mchungaji wao huku wakimkashifu kwa kupenda hela. Kisa hicho ambacho kiliwashangaza wengi, kilizuka baada ya mchungaji huyo ambaye ndiye mwenye kanisa hilo kuwakemea washirika wake kwa kutotoa sadaka wala fungu la kumi.

"Mchungaji huyo aliingia kanisani na kuwaambia washirika kwanza watoe sadaka na fungu la kumi, kabla ibada haijaanza." Alisimulia Ghost.

"Baada ya watu kutoa sadaka, kuna wengine ambao hawakutoa sadaka na hapo ndipo kisanga kilianza. Mchungaji huyo alianza kuwafokea kondoo wake. ''Hakuna haja ya kuja kanisani na hamtoi chochote, mnakujaje kujaza viti hapa mwakaa tu?" mchungaji alifoka." Na punde tu muumini mmoja aliposimama na kumkashifu mchungaji huyo kwa matamshi yake, alikipata cha mtema kuni.

Sikiza kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be