'Kama siasa ni ujanja unafanya vibaya,'Mutahi Ngunyi amwambia Martha Karua

Mchambuzi wa siasa Mutahi Ngunyi amemwambia Aliyekuwa waziri wa haki na mbunge wa Gichugu Martha Karua kwamba kama siasa ni ujnja anafanya vibaya sana.

Katika ushauri aliouita wa ujinga alisema kuwa Karua anapaswa kufanya wakenya na watu wampenda na wala si kumuogopa kama ni kesi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Mutahi alisema kuwa kiongozi huyo wa chama cha Narc Kenya anapaswa kutabasamu na kuwa na furaha wakati mwingine.

Mchambuzi huyo alijitolea kuwashauri Miguna Miguna na Karua cha kufanya ili waweze kupendeza wakenya na watu.

"Ushauri wa kijinga kwa Martha Karua, katika siasa unapaswa kutufanya tukupende na wala si kukuogopa unapaswa kutabasamu sana na kukasirika kidogo

Unapaswa kucheka na wala si kubweka, unapaswa kuonekana mwenye furaha na wala si mwenye amekasirika, na kama siasa ni ujanja unafanya vibaya sana

CPA James: Well said,we dont want those cosmetic smiles
 
Gitobu Kiogora: Karua looks Scary...That is mainly the reason why Kirinyaga residents voted Waiguru instead of Karua... Likeability is key