Kate Actress afichua sababu ya kutoka katika kipindi cha Mother-in-law

Catherine Kamau Karanja almaarufu, Kate actress, Celina na Sue aliweza kujulikana katika usanii kwa sababu ya kipindi cha Mother-in-law ambacho uwa kinaonyeshwa katika runinga ya Citizen.

Aliigiza katika kipindi hicho kwa muda wa miaka nane, kisha akatoka.

Alilelewa katika kijiji cha Nyambururu, alipoenda chuo kikuu nchini Uganda alibeba mimba na kisha kufukuzwa na wazazi wake kwa sababu ya mimba hiyo.

Baadaye waliweza kumkubali na kisha kumsaidia katika kumlea mtoto wake.

"Niliporudi kutoka Uganda nilikuwa na mimba wazazi wangu walipojua walinifukuza kisha baada ya muda ama baada ya kumaliza kukasirika,

"Walinisaidia katika kumlea mtoto wangu ambaye kwa sasa ako darasa la nane, kwanza mamangu amekuwa akinisaidia kumlea mtoto wangu sana.

"Nilieza kumuacha mtoto wangu nyumbani nikakuja Nairobi kutafuta kazi,wazazi wangu walinikataa kwa sababu waliona ni kama nimewakosea heshima katika jamii,"alieleza Kate.

Waliweza kupatana na mume wake akiwa katika kipindi cha Mother-in-law, ambaye alikuwa mwelekezi katika kipindi hicho.

Ameolewa na Phill Karanja, ambaye alimsifu kwa sana.

"Mara ya kwanza tulikuwa na marafiki wa karibu aliweza kunielekeza cha kufanya,kisha tukakua na uhusiano wa kimapenzi na tukaoana,ndio maana namuamini na ndoto zangu za maisha,

"Mume wangu tulipoanza uhusiano huo aliniambia nisibadilike kwa maana alinipata nikifanya vituko na uwa ana kubaliana na mimi kwa kila jambo,"Kate alizungumza.

Muigizaji huyo alisema kuwa anapenda kusaidia watu mahali anaweza kwa maana na moyo safi, Kate aliweza kubeba mimba yake akiwa na miaka 19.

Pia alieleza kuwa alitoka katika kipindi cha Moter-in-law kwa sababu alikuwa anataka kujikuza kwa mabo mengi.

"Niliacha kipindi cha Mother-in-law kwa sababu nilikuwa nataka kukuwa licha ya kukuwa nilikuwa nataka kufanya mambo mengi ambayo yangenisaidia maishani," Kate alisema.

Aliweza kusema uwa wanaongea na waigizaji wa kipindi hicho kwa sababu hakutoka kwa ubaya wowote.

"Uwa tunaongea na waigizaji wa Mother-in-law kwanza chali ni rafiki yangu sana,"alizungumza Kate.

Amefanya vipindi viwili Mother-in-law na Sue na Johnie. Ni mwenye kipindi cha Sue na Johnie baadaye kupatana na Abel Mutua akaandika kipindi hicho.

"Niliweza kuja na kipindi hicho cha lugha ya mtaani, yaani 'sheng', ili watu na vijana wengi wawe huru kufanya vipindi hivyo. Kwa sababu vipindi vingi vimefanywa na kiingereza na kiswahili sanifu na wengi wamelelewa katika mjini,"aliongeza Kate.

Catherine akiwa katika kipindi cha ilikuaje na Massawe Japanni alisema kuwa ameokoka na anampenda mungu licha ya uigizaji wake.

Katika picha ambayo aliweka katika mtandao wa kijamii kuhusu DK Kwenye Beat hakuwasaidia baada ya kusikia sauti ambazo zilitamba za DK wakiomba msamaha.

'Hakuna vile unaweza omba msamaha na kisha ikue ilikuwa mzaa ulikuwa unafanya 'I can't support that nonsense,' siwezi kuunga mkono tabia kama hiyo,"aliongezea Kate.