Kindiki,Murkomen na Cherargei watupilia mbali nyadhifa walizopewa na chama cha Jubilee

kindikiii11
kindikiii11
Hatua ya kuwatimua maseneta Kipchumba Murkomen, Kithure Kindiki na Samsom Cherargei kutoka kwenye nyadhifa zao sasa zimepanua nyufa katika chama tawala cha Jubille.

Hili limebainika baada ya Kithure kindiki wa Tharak Nithi, Kipuchumba Murkomen wa Elgeyo Marakwet na Samson Cherargei kutupilia mbali nyadhifa ambazo walikuwa wametengewa na chama hicho.

Kindiki ambaye alikuwa ameteuliwa katika kamati ya haki na sheria alitupilia mbali uteuzi huo akisema akili zake sasa zinaangazia tu utendakazi wake kwa wananchi wa Tharaka.

Kwa upande wa Cherargei ambaye alitimuliwa kama mwenyekiti wa kamati ya kuangazia sheria, alitupilia mbali wazo la kuteuliwa kama mmoja wa kamati ya  Powers and Privileges .

“I hereby write no notify you that I have declined the appointment to be a member of the Powers and Privileges Committee in the Senate,” alisema  Cherargei .

Murkomen, ambaye alitimuliwa kama kiongozi wa wengi kwenye bunge la seneti pia alikataa kuchukua wadhifa wa kuwa mwanachama wa kamati ya kuangazia ugatuzi nchini kama njia ya kuchukuwa nafasi ya seneta wa Laikipia John Kinyua.

“This afternoon I learnt from the media that I have been proposed to serve in the Senate Devolution Committee in effect replacing Senator Kinyua who is being punished for standing with me. Accepting the position will be tantamount to repaying unstinting loyalty with spite&treachery,”  Murkomen aliandika.

 Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi, kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Irungu Kang'ata, seneta wa Meru Lithika Linturi aliondolewa katika kamati ya uhasibu wa pesa za umma na nafasi yake kuchukuliwa na naibu kiranja wa wengi Fatuma Dullo.
Seneta wa Laikipia ni wa hivi maajuzi kutimuliwa na chama cha Jubilee kutoka kwa kamati ya ugatuzi nchini.