‘You Should Know People’ Mkuu wa Polisi wa Nandi ahamishwa.

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Nandi  Thomas Ngeiywo amehamishwa hadi makao makuu ya polisi wiki moja yake kushindwa kumzuia gavana wa kaunti hiyo Stephen Sang Kuvamia shamba la chai linalohusishwa na waziri wa zamani Henry Kosgey .

Bw. Ngeiywo  alitakiwa kurejea Nairobi wiki jana na mrithi wake kuthibitshwa siku ya jumanne . Nafasi yake itachukuliwa na  Samuel Ole Kine  ambaye alikuwa katika makao makuu baada ya  kutolewa   Trans Nzoia .

Bwana Kine alihudumu katika wadhfa kama huo kabla ya kuhamishwa . Maafisa wa usalama  huko Nandi wamethibitisha kwamba  Ngeiywo  alitakiwa kufika Jumba la Vigilance wiki jana  kufuatia tukio hilo ambalo baadaye lilisababisha gavana Sang kukamatwa na maafisa wa DCI na kufikishwa mahakamani Kisumu .