Kongole Sauti Sol! Watashirikiana na Radio Africa Group katika uzinduzi wao wa Albamu ya 5

Kikundi cha wanamziki wa humu nchini Sauti Sol watashirikiana na kampuni ya Radio Africa Group katika uzinduzi wao wa albamu yao ya tano kwa jina Midnight Train Juni 5.

Mashabiki wa kikundi hicho wataweza kupata ngoma zote kwenye albamu hiyo kwa kufuatilia vituo vya Classic 105, Smooth Fm, Kiss 100, Radio Jambo na Homeboyz Radio kuanzia Ijumaa asubuhi.

Wimbo wao Suzanna ambao ulizinduliwa Februari 6 uko na wafuatiliaji zaidi ya milioni moja kwenye Youtube.

Wamesema kutokana na vigezo vilivyowekwa na serikali kama vile kupiga marufuku usafiri wa ndege umechangia pakubwa biashara kurudi chini.

"It has forced us to not only postpone and/or cancel all local and international performances but also to isolate at a time we need to be together preparing for the launch and eventual performance and touring of our new album," wamesema Sauti Sol.

Wamesema ni maombi ya mashabiki wao kushuhudia uzinduzi wa Albamu hiyo kupitia kwa matumbuizi ama kuwa na hafla tofauti kando na changamoto ambazo zimekumba ulimwengu kwa sasa.

 "It is the expectation of our fans and stakeholders that we launch this album with a concert/performance regardless of the circumstances." wanmesema wasanii hao.