‘Kulikuwa na kitu kilichokosekana maishani mwangu’’ Avril azungumza kuhusu maisha yake ya mapenzi

Msanii Avril amezungumza   kwa mara ya kwanza kuhusu maisha yake ya mapenzi.

Katika mahojiano aya hapo awali nyota huyoalifichua jinsi ilivyuokuwa vigumu kwake kumkabali mwanamme katika maisha yake

Avril  amesema kifo cha babake kilimfanya asimuamini yeyote katika maisha yake lakini baadaye akakubali  kumruhusu baba ya mtoto wake katika maisha yake

Alisema kwamba alifanya kilaawezalo kuwafungia nje waliotaka kuwa katika uhusiano wa kimapenzi naye

“ Nilihoji nia ya kila mtu aliyekuja katika maisha yangu akidai kwamba ananipenda.Niliwafungia watu wengi nje ya moyo wangu’’

Aliongeza kwamba alijipata akitaka kusalia pekee yake bila kutaka kutangamana na mtu yeyote .

“ kwa kiasia ,hali hiyo ilinisaidia  ni jambo la kiajabu lakini kwa hatua Fulani niliweza kurejea katika fani ya usanii tena .Nilianza kujizatiti zaidi katika kazi zangu’’

  “ Nilitaka mtu tofauti ambaye hakuwa katika fani hii.so nliamua kuanza uhusianona mtu mmoja..Nina mtu kwa sasa katika maisha yangua ambaye tumepata mtoto  mvulana naye ,lakini bado nina maswali mengi’’ ameongeza msanii huyo

Kwa sababu ya maumbile yake ya kuuliza maswali Avrilanasema hali hiyoimesababisha  hali ya  kuwepo ugomvi wa kila mara na baby daddy wake .

“ Najipata nilihoji hata mapenzi yake ,utunzi wake  mjinsi mtu anavyoweza kukupenda tu bilamasharti.ni vipi mapenzi yasio na masharti hufanywa?

Avril   amedaiwa kwa muda mrefu sasa kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na muelekezi wa video J Blessing .wawili hao inadaiwa wapo katika penzi zito

Baada ya miezi kadhaa ya kuficha uhusiano wao  ,Avril hatimaye alijitokeza kutangaza mapenzi ayake kwa J  Blessing  wakati alipokuwa akisherehekea birthday yake kwa kuandika ;

“Happy Birthday . Thanking God for you ,”

Avril  kisha aliposti msururu wa picha zake na J blessing katika ukurasa wake wa instagram. Picha hizo ziliambatana na jumbe tam tam za mahaba