Leo ni siku ambayo tunasherehekea wafanyakazi wetu wote! Kenyatta asema

NA NICKSON TOSI

Leo ni siku ambayo tunasherehekea siku ya wafanyikazi dunia nzima lakini kwa sababu ya yale ambayo yamekumba nchi zote za dunia leo tunasherehekea kitofauti. Nachukua nafasi hii kuambia wakenya wote Happy Labour Day.

Ni usemi wa kiongozi wa taifa Rais Kenyatta akihutubia taifa katika maadhimisho ya leba dei ambayo huadhimishwa na wafanyakazi kote ulimwenguni.

Rais Kenyatta ameongeza kuwa yuko tayari kuhakikisha maslahi ya wakenya haswa kutokana na hasara kubwa iliyosababishwa na virusi vya corona kwa uchumi wa taifa.

Kenyattta ameongeza kuwa hawawezi kuangazia tu janga la corona wakati ambapo uchumi wa taifa ukiendelea kudorora kwani asilimia kubwa ya wakenya huenda wakapoteza ajiri.

Kinara wa taifa ameongeza kuwa ameamrisha wizara ya fedha kutenga pesa ambazo watu wasiojiweza kwa jamii na wakongwe wataanza kupokea kama njia ya kukimu mahitaji yao wakati huu.

Kenyatta pia ametoa wito kwa wakenya na kampuni za humu nchini kuendelea kununua bidhaa zinazo tengenezewa nchini kama mbinu ya kuinua uchumi wa taifa.

Wakati uo huo Uhuru amewaonya viongozi wanaoeneza siasa wakati huu ambapo serikali imeweka vigwazo kwa wananchi wake akisema sio wakati wa kueneza siasa japo kushirikiana na kufanya kazi.

Uhuru amewakemea wale wote wanaoshutumu hatua ya serikali ya kuendelea kutuma maua Uingereza akisema ni sharti uchumi wa taifa uendelee kuimarika.