Machozi ya mamba! Echesa arai mahakama kuruhusu apewe gari lake

Waziri wa michezo wa zamani Rashid Echesa ameiomba mahakama ya Nairobi kumruhusu aende kuchukua gari lake aina ya Range Rover baada ya kuzuiliwa kutokana na kesi za ufisadi zinazomkabili.

Echesa kupitia kwa wakili wake Bryan Khaemba ameiambia mahakama ya Milimani kuwa tangu gari lake kuchukuliwa Machi 2 mwaka huu, amelazimika kutumia magari ya uchukuzi wa ummaa kwa kusafiri.

Khaemba sasa ameenda kwa mahakama hiyo akisema kuwa huenda mteja wake ambaye ni Echesa akaambukizwa virusi vya corona kswa kutumia magari ya uchukuzi wa umma.

Katika ombi lake la Machi 11, Echesa aliitakja mahakama kuishauri afisi ya DCI kuachilia gari lake akisema kuwa kwa kuwa alikuwa waziri wa zamani huenda maisha yake yakawa hatarini kwa kuendelea kutumia usafiri wa umma.

“Let the vehicle and his firearms be released until the State is ready to respond to the application,” .“It is almost three months since the application was filed in court [and there is no progress on the matter]. It is against logic why the case was filed under a certificate of urgency,” amesema Khaemba.

Ameongezea kuwa Echesa amelazimika kukaa nyumbani kufuatia vitisho vya kila mara na kuhofia kuwa maisha yake yamo hatarini.