Madrid wana imani watamsajili Salah kwa kitita cha pauni 126M

salah
salah
Real Madrid wanaamini wataweza kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah, 27 kwa kitita cha pauni milioni 126 baada ya kuachana na mshambuliaji Gareth Bale, 30 (El Desmarque, via Express)

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho ana matumaini ya kuipiku Manchester United kumsajili kiungo wa RB Leipzig Emil Forsberg, 28. (Express)

Timu ya Serie A, Inter Milan imewasiliana na Tottenham kuhusu mchezaji wa nafasi ya ulinzi Jan Vertonghen, 32, ambaye bado hajakubali mkataba mpya. (Standard)

Manchester United wanajiandaa kumuuza kiungo Jesse Lingard, 27, na Andreas Pereira, 24, kwa ajili ya kugharamia uhamisho wa kiungo Jack Grealish,24. (Express)

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamekuwa katika mawasiliano na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firmino,28. (Echo)

Katika hatua nyingine, Liverpool wako kwenye mazungumzo na RB Leipzig na mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 23. (Express)

Kocha wa Inter Antonio Conte anataka kumnyakua mmoja wa mabeki wa kushoto wa Chelsea, kati ya Marcos Alonso, 29 na Emerson Palmieri, msimu huu. (Tuttosport, via Mail)

Mshambuliaji wa Chelsea Willian, 31, anasema mkataba wa sasa wa klabu hiyo haujakidhi matakwa yake hali itaja kuwa ''ngumu''. (Esporte Interativo, via Football 365)

Roma inataka kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi Chris Smalling, 30, na kiungo Henrikh Mkhitaryan, 31, kwa mikataba ya kudumu. wawili hao wanacheza kwa mkopo wakitokea Manchester United na Arsenal. (Sky Sports)