Majuto:Makosa na utepetevu ambao huenda ukatugharimu maisha katika vita dhidi ya Coronavirus

Huku ulimwengu mzima ukiendelea kupambana na virusi vya Corona ambavyo vimesababisha vifo vya watu   zaidi ya 13,000 na wengine 308,564 kuambukiwa ,kuna  baadhi ya wakenya ambao wamechukulia janga hilo kama mzaha .

Jinsi wanavyochukulia kwa wepesi janga la virusi hivyo ndivyo jinsi Italia ilivyofanya mwanzoni kabla ya kupigwa na uhaliasia wa mambo na sasa ndio taifa lenye maafa mengine wa Corona hata kuliko China ,chimbuko la ugonjwa huo . Kufikia  jumapili ,watu 4825 nchini  Italia walikuwa wamekufa kwa ajili ya virusi vya Corona ikilinganishwa na watu 3261 walioaga dunia nchini China . Je,ni makosa yepi ambayo Italia ilifanya ? Je,wangefanya nini tofauti ambayo tunafaa kujifunza na kutekeleza ? Hii hapa orodha ya  baadhi ya mambo tunayofanya ambayo huenda yakatupa machozi

  1. Wahudumu wengi wa matatu hawana maji/sabuni au vitakasa mikono/wanachukua pesa taslimu

Katika baadhi ya vituo vya magari wasafiri na wahudumu wa matatu wanaendelea  na shughuli zao kama kawaida.hakuna anayejali kuhusu usafi au hata hofu ya virusi vya Corona . Wengine wanalichukulia suala zima kama utani mkubwa . maambukizi ya virusi hivyo yanaweza kusambazwa pakubwa n usafiri wa PSV na sekta hiyo ingekuwa ya mwanzo kuchukua tahadhari .  Baadhi yao pia wamekataa kuchukua pesa za nauli kupitia mfumo wa simu na wanataka pesa taslimu . Shirika la afya duniani WHO limesema virusi vya Corona vinaweza kusambazwa kupitia noti na sarafu zinazokabidhiwa mtu mmoja hadi mwingine .wahudumu wa matatu wanataka ‘cash’ na hawataki  mzaha .

  1. Wenye Biashara kupuuza  kuweka maji na vitakasa miko nje ya biashara zao

Kote nchini kuna watu waadilifu na wanaofahamu  matokeo ya utepetevu na hivyo basi wameweka mikakati yakuhakikisha usafi unadumishwa .katika biashara ndogondogo hata mitaani kuna wafanyibiashara walioweka vibuyu vya maji na sabuni kwa wateja kuweza kunawa mikono .Hata hivyo kuna wengi ambao wamepuuza hilo na wanaviona vitu hivyo kama maua na mchezo .  Ukosefu wa kutekeleza  hatua hiyo pia umechangia uzembe.

  1. Kwenda maeneo ya watu wengi /Mabaa/ Mikutano

Licha ya agizo  na  himizo la serikali kwa watu kuepuka maeneo yenye watu wengi ,kuna wenye viburi ambao  ushauri  wanausikia lakini kamwe hawafuati  maagizo ,hata kwa usalama wao! Kabla ya kuagizw akwa mabaa kufungwa saa moja unusu jioni ,maeneo mengi ya burudani yamekuwa yakishuhudiwa wateja wengi waliofurika sehemu hizo wakiendelea na ulevi wao . Inakuwa vigumu wewe kujikinga dhidi ya irusi hivyo iwapo umelewa na huna ufahamu wa kilicho sawa na kisicho .Iwapo lazima ulewe umeshauri kununua kileo chako uburudikie nyumbani . Kuna wanaoendelea na mikutano ya watu wengi na maajuzi nimeona tawi la kilabu moja ya soka nchini   likifanya mkutano na wa mashabiki wake !

  1. Kusafiri kusiko kwa lazima

Baada ya shule kufungwa kuna  watu ambao lazim wangesafiri kwenda nyumbani –wanafunzi,walimu na kadhalika .Lakini kun watu wanaotumia fursa hii kusafiri kwenda mashambani! Hawqana shughuli muhimu huko lakini kwa sababu wamepata muda basi wamepiga folenikatika vituo vya magari kwenda nyumbani .Sasa hatari ni iwapo una virusi hivyo basi utawaambukiza jamaa zako wote huko mashambani ! salieni mliko hadi  virusi hivi vidhibitiwe .

  1. Fanyieni kazi nyumbani ,sio kuitana nyote katika  nyumba ya mmoja wenu!

Waaajiri wengi wamehimiza kuwaruhusu wafanyikazi wao kufanyia kazi nyumbani .hii ni kuzuia  utangamano wa watu wengi katika nafasi ndogo za afisini .Lakini kuna werevu waliopewa fursa hiyo ambao sasa wakiwa mitaani ,wameitaka ktika nyumba ya mmoja wao ili kufanyia kazi huko! Dhamira ilikuwa kuzuia mrundiko wa watu mahali pamoja na sasa mkifanya hivyo  ni heri basi mgenfanyiakazi afisini .

 Feki,feki ,feki kila kitu feki!

Wakenya  ni watu wazuri lakini wakati mwingine tamaa yao na  ujinga wao hauwezi hata kukadirika .Kumetangazwa janga la dharura  lakini kuna werevu waliomua kutengeza  sanitizers feki ambazo wanawauzia watu.Unapoteneza bidhaa kama hiyo  feki isofanya kazi ,unahatarisha hata maisha yako kwa sababu maambukizi yakilipuka ,hata wewe utaathiriwa .Sasa ukiwauzuia watu bidhaa feki ,kisha waambukizwe na wafe  wote ,utamuuzia nani baadaye?  Kingine kinachoghadhabisha ,ni kuongeza gharama ya biadhaa muhimu .Maajuzi sabuni na bidhaa zote za kuosha mikono zilikuwa za gharama ya kwaida .Sasa baadhi ya bidhaa hizo za usafi zinagharimu zaidi kuliko hata chakula!