Mali ya SDA Ibara yaporwa, Divai takatifu na mkate wa ekaristi havipo

unnamed
unnamed
Waumini katika kanisa la SDA Ibara waliamukia tukio la kushangaza baada ya wezi kuvamia kanisa lao na kufagia kila kitu.

Washukiwa wa wizi Ijumaa walivunja kanisa la SDA Ibara lililopo kaunti ya Nyamira na kutoroka na divai takatifu pamoja na mkate wa ekaristi.

Wezi hawa hawa pia walitoroka na vifaa vya kumtukuza Mungu zikiwemo spika na viti vya kanisa.

Soma hadithi nyingine:

a

Waumini walirudi nyumbani huku wamekasirika baada ya kukosa mkate na divai kufuatia wizi huo.

Viongozi wa kanisa wanahoji kwamba walifahamu kuhusu wizi huo asubuhi ya Jumamosi kipindi wakitayarisha ibada.

"Milango ya mbele na nyuma imevunjwa. Wezi walifagia kila kitu huku ndani." Alisema mzee wa kanisa Evans Ariga.

Ibada ya Jumamosi ilifanyika nje.

Kanisa la SDA huwa na ibada ya ekaristi mara moja baada ya miezi 3 kulingana na ratiba yao ya mwaka.

Soma hadithi nyingine:

Ariga amesema kuwa walipiga taarifa katika kituo cha polisi Keroka kuhusu tukio hili.

"Tumeripoti kwao ili wafanye uchunguzi. Ila kwa misingi ya ukristo, tunaomba aliyefanya kitendo hiki aguswe na roho mtakatifu. Mwanzo atubu na arudishe alichoiba bila hivo ataishi kwa laana." Alisema Ariga