Mapigano Narok! maafisa zaidi wa polisi washika doria

Serikali imetuma vikosi zaidi vya polisi katika kaunti ya Narok kutuliza mapigano ya kikabila baina ya jamii za Kipsigis na Maasai katika kaunti ndogo ya Narok Kusini.

Soma pia;

Hali ya taharuki ilikuwa imetanda katika eneo hilo siku ya Jumatano baada ya Kamishna wa kanda ya Rift Valley George Natembeya kuzuru eneo la mapigano.

Soma pia;

Naibu Kamishna wa kaunti ya Narok Felix Kisalu alisema kwamba hali ya taharuki ilitanda eneo hilo baada ya baadhi ya wakaazi wa eneo la Olmegenyu, Sogoo, Segamian, Torokiat, Triangle na Nkoben kupiga mayowe.

“Tunafuraha kwamba hali ya utulivu imerejea baada ya vikosi vya usalama kuingilia kati ili kutuliza uhasama uliokuwepo,” Kisalu aliambia wanahabari afisini mwake siku ya Alhamisi.

Aliongeza kuwa watu wawili walikuwa wamekamatwa kwa madai ya kupiga kamza bila sababu.

Soma pia;

“Ikiwa kuna hali ya dharura piga ripoti kwa chifu au polisi badala ya kuanza kupiga nduru na kuzua hofu isiyofaa miongoni mwa jamii zinazoishi kwa amani,” alisema.

Mapigano yalizuka katika maeneo ya Olooruasi na Olpusimoru Narok Kusini na Kaskazini mtawalia. Jumla ya watu wanane wameuawa na wengine 13 kujeruhiwa vibaya tangu kuzuka kwa makabiliano hayo Ijumaa iliyopita.