"Marie-Rose aanza shule, tunamshukuru mungu" - Gidi

Tangu kuzaliwa kwake mwanawe Gidi, Marie-Rose, tumekuwa tukifuatilia kwa kina jinsi anavyokua na kila anacchofanya, hii ni kwa hisani ya picha na video zinazo chapishwa na bwana Gidi.

Gidi hajakuwa studioni tangia jumatatu na Ijumaa iliyopita alitangaza kuwa atakuwa akizuru miji mitatu mikuu duniani katika pilka pilka za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Gidi husherehekea siku ya kuzaliwa tarehe 5 kila Septemba. Tayari ametembea mji wa London ambapo alipata fursa ya kutizama mechi kali kati ya Arsenal na Tottenham.

Masaa machache baadaye alisafiri hadi Ufaransa na kupatana na familia yake inayoishi humo.

Siku moja baadaye, Gidi pamoja na mkewe walishuhudia siku ya kufana kwani baada ya kuwa katika shule ya chekechea kwa miaka mitatu, Marie-Rose alianza shule rasmi.

Wazazi wake walikuwa na wingi wa furaha, na huku akiwa amejihami na suti na tai, Gidi hakusita kuchapisha picha za familia hiyo shuleni humo.

Gidi aliandika,

After 3 years at the day care, Marie-Rose starts her formal education today. We thank God for this special day🙏🙏🙏

Mwenzake Ghost Mulee na rafikiye Chris Kirwa walikuwa miongoni mwa waliompongeza bwana Gidi.

Ghost Mulee: Congratulations Leo buda umekauka

Chris Kirwa: She made you wear a suit 🔥🙌💪😀😀 Marie for President 😀

LInda Muhaya: All the best to the little angel

Odera: I like the way you treat your family. ..you're such a gentleman with a family bond

Frank Nyabuga: Mkuu WA patanisho naona ukona Familia smart