Masaibu ya Timmy T Dat, BASATA yamjia juu Rosa Ree kisa video chafu

timmy-tdat-ft-rosa-ree-–-vitamin-u
timmy-tdat-ft-rosa-ree-–-vitamin-u
BASATA ambayo ni bodi ya kutathmini ubora wa sanaa nchi jirani Tanzania imemfungia staa wa kike Rosa Ree nje ya gemu kwa kipindi cha miezi 6.

Haya yanajiri baada ya mwanadada huyu kuonekana katika video chafu ya Vitamin U.

Nyimbo hii pia ilifungiwa nchini Kenya na bodi ya filamu.

https://www.instagram.com/p/B4y503LnCys/

Katika video hiyo, vipo vipande Timmy T Dat alionekana akishika matiti ya mwanadada huyu.

Aidha, mtandao wa YouTube uliweza kuitoa video hii na Insta ya Timmy T Dat kufungwa.

Timmy hakuweza kushika simu yetu ili kuweza kuzungumzia akaunti ya Insta kufungwa.

Aidha, hajaweza kutokeza na kueleza bayana kuwa yeye ndiye alifuta wimbo huo ama ni YouTube wenyewe.

Kwa mujibu wa kaimu katibu mkuu wa BASATA Onesmo, msanii huyo anatakiwa kutoa faini ya Tsh 2 M (Khs 88,671.50)