Massawe atarudi kuwapasha polisi Industrial

26871269_2014344865488048_5223969422204469248_n
26871269_2014344865488048_5223969422204469248_n
Baada ya ajali ya jumatano iliyofanyika kati ya gari ya staa wa redio Massawe na basi ya sacco ya Orokise, mtangazaji huyu ameapa kufika kituo cha polisi Industrial na kuwapasha.

Akizungumza jana katika kipindi anachopeperusha kuanzia saa nne hadi saa nane alasiri, mtangazaji huyu alionekana kutopendezwa na wanapolisi hao.

"Am still going for my abstract and I think I will give them peace of my mind." afoka Massawe.

Soma hapa:

Massawe akionekana kukerwa na tabia ya wanapolisi hao, amefunguka walivyomnyamazisha na kumtaka asiongee. Alikuwa ameandamana na maafisa wa polisi hadi kituo hicho baada ya tukio hilo.

Massawe aligongwa na gari kutoka nyuma na kuvunja kioo cha gari lake. Kulingana naye gari hiyo ya sacco ya Orokise ndio walivunja sheria za barabarani.

"Unajua wakati mwingine unaweza ukawa careful barabarani lakini mwenzako hafuati sheria."

Baada ya kupatikana na bima pana ya gari lake, afisa mmoja alimueleza kuwa asiwe na hofu.

Pata uhondo hapa:

"Madam insurance yako ni comprehensive wacha insurance isort." amesema Massawe.

Hali kadhalika Massawe amedokeza alivyotaka kukimbia na kutoweka baada ya kisa hicho lakini msamaria mwema akamsihi asifanye hivyo.

"Nilitoka mbio. Nilikuwa nataka kutoroka. Msamaria mwema akaniambia nisifanye hivyo."

Massawe ameongeza kusema kuwa wanapolisi hawafai kuwadhulumu wananchi na kuwa uwepo wao ni kuhakikisha usalama kwa watu wote.