Miaka 50 gerezani kwa mwanamume aliyemnajisi mtoto wa mwaka mmoja

Mwanamume mwenye umri wa miaka 20 atalazimika kukaa gerezani kwa kipindi cha miaka 50 baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi matoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja katika kaunti ya Mandera.

Mahakama siku ya Ijumaa ilimhukumu jamaa huyo aliyekuwa tayari kapatikana na hatia ya kumtendelea unyama malaika mwenye wa mwaka mmoja.

Akitoa uamuzi wake hakimu mkuu Kimani Mukabi alisema kwamba ilithibitishwa kuwa mshukiwa alikuwa ametendea unyama mtoto huyo na kumharibia maisha na hivyo kustahili adhabu kali ili liwe funzo kwa wengine.

Alisema hukumu ya miaka 50 gerezani ni adhabu tosha kumpa haki mhasiriwa.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Charles Mogaka ulifanikiwa kushawishi mahakama kuwa mshukiwa alitenda kosa hilo.