Olivier Giroud ahamia AC Milan kutoka Chelsea

Giroud alichezea Arsenal kwa kipindi cha miaka tano

Muhtasari

•Giroud atavaa jezi nambari tisa huko AC Milan.

Image: TWITTER//AC MILAN

Mshambulizi wa Ufaransa Olivier Giroud amekamilisha uhamisho wake kutoka Chelsea kwenda AC Milan.

Giroud, 34, ametia mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Italia baada ya kusajiliwa kwa  pauni milioni mbili.

Mshambulizi huyo ameichezea Chelsea kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu kufuatia uhamisho wake kutoka kwa klabu hasidi ya Arsenal mwaka wa 2018.

Kabla ya kujiunga na Chelsea Giroud alichezea majirani Arsenal kwa kipindi cha miaka mitano na nusu.

Giroud atavaa jezi nambari tisa huko AC Milan.