Tetesi za soka Ulaya: Hali ilivyo kwenye dirisha la uhamisho Jumatatu tarehe 26.07.2021

Manchester United inakaribia kufikia makubaliano na Real Madrid kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, 28, kwa dau la £42m

Muhtasari

•United pia wanaweza kumsajili kiungo wa hispania Saul Niguez kutoka kwa mabingwa wa La Liga Atletico Madrid kwa dau la £45m. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anahusishwa pia na vilabu vya Barcelona na Juventus

•Juventus imepanga kufanya mazungumzo mengine mapya na Sassuolo wakipambana kumshawishi kungo wa Italia Manuel Locatelli anayewaniwa pia na klabu ya Arsenal.

Raphael Varane
Raphael Varane
Image: REUTERS

Manchester United inakaribia kufikia makubaliano na Real Madrid kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, 28, kwa dau la £42m. (Marca)

United pia wanaweza kumsajili kiungo wa hispania Saul Niguez kutoka kwa mabingwa wa La Liga Atletico Madrid kwa dau la £45m. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anahusishwa pia na vilabu vya Barcelona na Juventus. (Mail)

Borussia Dortmund wanaonekana kukamilisha mpango wa kumsajili nyota anayewaniwa na Liverpool Donyell Malen, 22 kwa dau la £26m. Wanamuona mshambuliaji huyo wa PSV Eindhoven na timu ya taifa ya Uholanzi kama mbadala wa mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 21 aliyetimkia Manchester United. (Fabrizio Romano)

Eric Lamela
Eric Lamela
Image: REUTERS

Winga wa Argentina Erik Lamela, 29, anakaribia kukamilisha uhamisho wake kutoka Tottenham kwenda Sevilla, huku Winga wa Hispania Bryan Gil, 20, akielekea upande wa pili. (Marca)

Newcastle watamgeukia kiungo wa Chelsea na England Ross Barkley, 27, kiwapo watashindwa kumsajili Joe Willock, 21, kutoka Arsenal. (The Athletic - subscription required)

Juventus imepanga kufanya mazungumzo mengine mapya na Sassuolo wakipambana kumshawishi kungo wa Italia Manuel Locatelli anayewaniwa pia na klabu ya Arsenal. (Goal)

Kalidou Koulibaly
Kalidou Koulibaly
Image: GETTY IMAGES

Paris St-Germain wamefanya mazungumzo na wakala wa Kalidou Koulibaly katika harakati zao za kumsajili mlinzi huyo wa Napoli and Senegal mwenye umri wa miaka 30 (Corriere dello Sport - in Italian)

Kiungo wa Uhispania Isco, 29, hatapewa mkataba mpya na klabu yake ya Real Madrid. Mkataba wake wa sasa unamalizika msimu ujao. (AS - in Spanish)

Kiungo wa Chelsea na Scotland Billy Gilmour, 20, ameonyesha kipaji chake cha sauti kwa kuimba karaoke classic katika mgahawa mmoja huko Norwich, ambapo yupo huko kwa mkopo. (Sun)

Paul Pogba
Paul Pogba
Image: GETTY IMAGES

Meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer anataka kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, 28, kubakia katika klabu hiyo, huku Paris St-Germain ikimtaka . (Manchester Evening News)

Arsenal, Tottenham na Everton wanangalia uwezekano wa kumchukua kiungo wa safu ya ushambulizi Muargentina Joaquin Correa, 26, ambaye anatarajiwa kuondoka Lazio msimu huu . (Corriere dello Sport)

Juventus wamekataa dau la pauni milioni 86 kutoka kwa Liverpool kwa ajili ya Federico Chiesa. Winga huyo mwenye umri wa miaka 23,alikuwa mchezaji nyota wa Italia katika Euro 2020. (Repubblica)

Kiungo wa kati wa PSG na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, anasema "hakuhisi kupendwa" na mitandao ya kijamii ilianza kumkosoa kabla ya kuondoka kwake kutoka Liverpool mwezi Juni. (Observer)