Embolo akataa kusherehekea baada ya kuifunga Cameroon, nchi yake ya kuzaliwa

Japo ana asili ya Cameroon, Embolo alikuwa anaiwajibikia Switzerland katika mashindano ya kombe la dunia Qatar.

Muhtasari

• Uswizi kwa sasa wanashikilia uongozi katika kundi G kwa pointi tatu huku wakisubiria mechi dhidi ya Brazil na Serbia.

Mshambulizi wa Uswizi, Breel Embolo akikataa kusherehekea kuifunga Cameroon, timu ya asili yake
Mshambulizi wa Uswizi, Breel Embolo akikataa kusherehekea kuifunga Cameroon, timu ya asili yake
Image: Twitter

Kiungo mshambuliaji wa Switzerland, Breel Embolo alikataa kusherehekea bao lao baada ya kuifunga Cameroon katika mechi yao ya kwanza ya kombe la dunia inayoendelea huko Qatar.

Itakumbukwa mshambualiaji huyo wa timu ya Ufaransa ya AS Monaco ana mizizi yake kutoka Yaounde nchini Cameroon lakini wazazi wake walihamia Uswizi wakati angali mdogo, na hivyo kuamua kuchukua urais wa Uswizi kuitumikia hata timu ya taifa.

Za ndani zinasema kuwa Embolo alijaribu kushawishiwa kubadilisha urais wake kuja Cameroon ili kuitumikia timu ya taifa ya miamba hao wa Afrika lakini alifanya uamuzi wa kusalia tu kama rais wa Uswizi.

Katika mechi yao ya kwanza kabisa kufungua kampeni za kusaka ubingwa wa kombe la dunia iliyowakutanisha Uswizi na Cameroon alasiri ya Alhamisi, kiungo wa kati wa timu ya Arsenal Granit Xhaka alimpa Embolo pasi nyerezi na kutia mpira wavuni, katika bao pekee la mchezo huo lililowapa Uswizi mwanzo wa aina yake katika mashindano hayo.

Kilichowashangaza wengi ni baada ya mchezaji huyo kukataa kushangilia kufunga bao hilo alilolifunga dakika tatu tu baada ya kurejea kwa kipindi cha pili cha mchezo.

Balada yake, Embolo alisimama tisti kama mlingoti na kuinua mikono yake juu huku amenyosha vodole angani huku wachezaji wenzake wakishangalia kwa vifijo na furaha isiyo na kifani.

Uswizi kwa sasa wanashikilia uongozi katika kundi G kwa pointi tatu huku wakisubiria mechi dhidi ya Brazil na Serbia.