Mbappe amtakia Pele kupona kwa haraka huku akivunja rekodi yake

Pele alikuwa ameshikilia rekodi ya kufunga mabao 7 akiwa chini ya umri wa miaka 24.

Muhtasari

• Mbappe baada ya kufunga mabao 2 dhidi ya Poland, alifikisha mabao 9 katika kombe la dunia akiwa bado hajafika umri wa miaka 24.

Kiungo mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe.
Kiungo mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe.
Image: Getty Images

Kiungo mshambulizi wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe ametoa wito kwa ulimwengu na mashabiki zake kumuombea aliyekuwa mshambuliaji matata wa Brasil, Pele.

Wikendi, majarida mbalimbali yaliripoti kuwa hali ya afya ya mkongwe huyo wa soka inazidi kuzorota kila uchao na kuwa alikuwa amehamishwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi zaidi wasiojua mchana wala usiku baada ya matibabu kushindwa kutoa majibu stahiki.

Baada ya kufunga mabao mawili na kuiwezesha Ufaransa kuinyuka Poland mabao matatu kwa moja, Mbappe alivunja rekodi ya kuwa mchezaji kinda mwenye umri wa miaka chini ya 24 kufunga mabao 9, rekodi ambayo ilikuwa imeshikiliwa na mkongwe Pele aliyefunga mabao 7 kabla ya kufika miaka 24.

Kabla ya mechi hiyo, aliwaomba watu kuzidisha maombi yao kwa Pelle ambaye kwa mara kadhaa amekuwa akidokeza kuwa ndiye himizo lake kubwa katika ulimwengu wa soka.

“Ombea mfalme Pele,” Mbappe aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Pele, mmoja wa wanasoka hodari zaidi kuwahi kucheza mchezo huo, aliiongoza Brazil kutwaa mataji matatu ya Kombe la Dunia mwaka wa 1958, 1962 na 1970. Anasalia kuwa mfungaji bora wa Brazil akiwa na mabao 77 katika michezo 92.

Wachezaji na mashabiki katika Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar hawakuwa na wasiwasi haraka mara tu habari za afya ya mwanasoka huyo wa Brazil zilipoibuka wiki hii.

Siku hiyo hiyo, Mnara wa Mwenge wa Doha ulimulikwa kwa taswira kubwa ya uso wa Pele pamoja na ujumbe "upone haraka".