Mourinho ailifananisha kazi yake AS Roma kama muujiza wa 'Yesu kutembea Vatican'

Mourinho alisema kwamba utakuwa muujiza mkubwa endapo ataingia Champions League na Roma kwani timu hiyo ilitumia €7M pekee kwa usajili mwanzoni mwa msimu.

Muhtasari

• Roma sasa hivi wako mbioni kujaribu kumaliza katika nafasi ya nne bora kwenye msimamo wa ligi ya Serie A.

• Pia timu hiyo imetinga kwenye fainali ya ligi ya Uropa ambapo kuna uwezekano mkubwa kufaulu Champions League ikiwa wataibuka mabingwa.

Mourinho ailinganisha kazi yake Roma kama Yesu kutembea Vatican
Mourinho ailinganisha kazi yake Roma kama Yesu kutembea Vatican
Image: Twitter

Kocha wa Roma, Mreno Jose Mourinho amesema haikuwa lengo la timu hiyo kufuzu kwenye michuano wa Champions League msimu kesho na endapo hilo litafanikiwa basi utakuwa kama muujiza mkubwa wa Yesu Kristu kutua katika mji wa Vatican na kutembea.

“Nani alisema Ligi ya Mabingwa ilikuwa lengo la Roma? Hakika sikufanya hivyo. Huwa najaribu kuwa mkweli, sipendi kuuza hewa moto, sikuwahi kusema Roma walikuwa mgombea wa nafasi za Ligi ya Mabingwa. Unaposhindana na timu zilizo mbele yetu, itakuwa ni kutowajibika kuzungumzia Ligi ya Mabingwa. Sikuwahi kufanya hivyo,” Mourinho alisema.

Mourinho ameingoza timu ya Roma mpaka sasa kushikilia nafasi ya sita kwenye ligi ya Serie A huku mechi chache ziliwa zimesalia na kuna uwezekano wa timu hiyo kumaliza kwenye nne bora na hivyo kujikatia tikiti ya Champions League.

Pia, Roma walitinga Fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Sevilla.

Zote mbili ni njia za kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao, lakini Mourinho kwa kawaida alikuwa na ugomvi katika mkutano wake na waandishi wa habari alipoambiwa kwamba hilo ndilo lengo lao la msimu wao.

Kulinagana na Mreno huyo, timu yake haikutarajiwa kabisa kuwa ingekuwa mshindani wa kuwania kumaliza nne bora na kufuzu ligi ya mabingwa kwani uongozi haukutumia kiasi kikubwa cha pesa kuleta sajili zenye nguvu.

“Tunaweza kuandika historia na kutaka kuendelea kuifanya, lakini kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wakati tunatumia €7m kwenye soko la uhamisho ni zaidi ya historia, zaidi ya muujiza. Ni Yesu Kristo akija Roma na kuwa na matembezi kuzunguka Vatikani," Mourinho alisema.

Mourinho alisema kuwa akifika kwenye ainali huwa habahatishi kwani anajua amebeba ndoto za watu wengi sana wakiwemo wachezaji wake ambao baadhi yao huwa ni fainali moja na ya mwisho kwenye maisha yao.

“Kitu pekee ninachopigania kwenye Fainali ni Fainali. Kuna makocha, wachezaji, vilabu ambao hucheza Fainali moja tu ya Uropa katika maisha yao na wanajiona wana bahati. Tunacheza mechi yetu ya pili mfululizo. Huu ni msimu mzuri kwangu, utakuwa wa kihistoria bila kujali kitakachotokea.”