Maguire atishia kuondoka Man Utd iwapo hatapewa muda mwingi wa kucheza

Lisandro Martinez na Raphael Varane ni miongoni mwa mabeki tegemeo ambao wamekuwa wakikabiliwa na majeraha, hivyo kumfanya Ten Hag kutokuwa na budi ila kumchezesha Maguire.

Muhtasari

• Hata hivyo, hoja ya uhamisho iliyopendekezwa ilishindikana, huku Maguire akijitokeza kudai kuwa 'hakukuwa na makubaliano yoyote' kuhusu masharti yake ya kibinafsi.

Harry Maguire adhibitisha kupokonywa unahodha wa United.
UNAHODHA Harry Maguire adhibitisha kupokonywa unahodha wa United.
Image: INSTAGRAM

Beki aliyekuwa nahodha wa timu ya Manchester United Harry Maguire ametishia kuigura timu hiyo iwapo ataendelea kuketishwa kwenye benchi na kocha Erik Ten Hag.

Maguire alikaribia kuondoka Old Trafford majira ya joto, huku West Ham United wakikaribia kumnasa kutoka United.

Kwa mujibu wa jarida la Metro UK, Maguire alifanikiwa kucheza mechi nane pekee za Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita, huku mechi zake nyingi zikitokea msimu huu kutokana na majeraha ya wachezaji wengine muhimu.

Hilo, kulingana naye linaelekea kumharibia hata muda wake wa kuitwa kwenye kikosi cha Three Lions cha Uingereza na hivyo mwezi Janauri katika dirisha fupi la uhamisho uenda akafanya uamzui mgumu wa kuondoka Old Trafford.

"Sitakaa hapa maisha yangu yote na kucheza mara moja kwa mwezi. Ikiendelea nina uhakika mimi na klabu tutakaa na kuzungumza kuhusu mambo," alisema.

"Nina imani na uwezo wangu na imekuwa ngumu. Nataka kucheza michezo na kujisikia muhimu kwa klabu. Kwa sasa, sijacheza popote karibu kama ningependa. Huo ndio msingi," aliongeza.

Kwa mujibu wa BBC Sport, ada ya pauni milioni 30 ilikuwa imekubaliwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu hiyo ya London.

Hata hivyo, hoja ya uhamisho iliyopendekezwa ilishindikana, huku Maguire akijitokeza kudai kuwa 'hakukuwa na makubaliano yoyote' kuhusu masharti yake ya kibinafsi.

Lisandro Martinez na Raphael Varane ni miongoni mwa mabeki tegemeo ambao wamekuwa wakikabiliwa na majeraha, hivyo kumfanya Ten Hag kutokuwa na budi ila kumchezesha Maguire.