Kevin De Bruyne aonekana msikitini Abu Dhabi kukiwa na tetesi za kuhamia ligi ya Saudia

Mkataba wa Mbelgiji huyo na Manchester City unamalizika 2025, ambayo ina maana kwamba kiungo huyo atahitaji kuangalia mahali pengine ili kutathmini mustakabali wake ujao

Muhtasari

• Mkataba wa Mbelgiji huyo na Manchester City unamalizika 2025,.

• Klabu mbili kutoka viwango tofauti vya Ligi za Saudi zimeripotiwa kuonesha nia ya kumnunua nyota huyo wa Manchester City ili kupata saini yake kwa msimu wa 2024-25

KEVIN DE BRUYNE KWENYE JOHO LA KIISLAMU
KEVIN DE BRUYNE KWENYE JOHO LA KIISLAMU
Image: X//CITYXTRA

Mchezaji nyota wa Manchester City Kevin De Bruyne alitembelea Msikiti Mkuu wa Sheikh Zayed huko Abu Dhabi siku ya Ijumaa, wakati wa ziara ya timu hiyo katika Falme za Kiarabu.

Wakati wa mapumziko ya msimu wa baridi wa Premier League, kikosi cha Manchester City na meneja Pep Guardiola walisafiri kwa ndege kwenda Abu Dhabi siku ya Alhamisi.

Timu hiyo itakuwa na mapumziko mazuri katika maeneo yenye jua kali ya Abu Dhabi kabla ya kurejea nyumbani kucheza na Spurs wiki ijayo katika mechi ya Kombe la FA.

Mapema mwezi wa Disemba, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 pia alitembelea shule za jiji la Abu Dhabi na kukaa kwa muda na wachezaji wa shule ya jiji, ambapo alipokea mapokezi makubwa kutoka kwa watoto wa shule.

Inasemekana kwamba Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF) umeonyesha nia ya kumnunua supastaa huyo wa Ubelgiji na amekuwa akiwasiliana na wachezaji.

PIF inamchukulia kama shabaha yao kuu ya Ligi ya Saudi Pro katika msimu wa joto wa 2024.

Mkataba wa Mbelgiji huyo na Manchester City unamalizika 2025, ambayo ina maana kwamba kiungo huyo atahitaji kuangalia mahali pengine ili kutathmini mustakabali wake ujao.

Klabu mbili kutoka viwango tofauti vya Ligi za Saudi zimeripotiwa kuonesha nia ya kumnunua nyota huyo wa Manchester City ili kupata saini yake kwa msimu wa 2024-25. Mmoja wao ni klabu yenye nyota wengi ya Al Nassr na klabu ya daraja la pili ya Al-Qadsiah.

De Bruyne, 32, alirejea hivi majuzi kwenye kikosi cha siku ya mechi dhidi ya Sheffield United mwezi Desemba. Alipata jeraha la misuli kwa muda mrefu katika mchezo wa ufunguzi wa msimu na kufanyiwa upasuaji.

Kiungo huyo aliyeshinda mara tatu amecheza mechi moja pekee Manchester City katika kampeni hii na kulingana na mwanahabari Rudy Galetti, mustakabali wake katika klabu hiyo bado haujulikani baada ya vilabu vya Saudia kumtaka.