Mkewe Nameless ajipata pabaya barabarani, aburuzwa korti ya Milimani

Wahu-cry-696x357
Wahu-cry-696x357
Mkewe Nameless leo amejipata pabaya barabarani baada ya kushikwa na maafisa wa trafiki.

Kwa mujibu wa maafisa hao, Wahu alivunja sheria za barabarani.

Mkewe Nameless aliburuzwa mahakama ya Milimani ili kujibu mashtaka.

https://www.instagram.com/p/B497TjSAheU/

Wahu alihesabiwa makosa ya kutatiza waendesha magari, kuendesha bila leseni pamoja na kupita waendeshaji magari katika hali ya kuhatarisha.

Mkewe Nameless hakuwa amebeba stakabadhi za kuonyesha kuwa ana leseni ya kuendesha gari wakati huo.

Mkewe Nameless alikuwa akiendesha gari lake barabara ya Ring Road wakati wa Asubuhi.

Hatimaye Wahu amekanusha madai hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya elfu 15.