'Jowie alikuwa afisa wa Interpol' shahidi adai katika kesi ya mauaji dhidi ya Jowie

Jowie-compressed (1)
Jowie-compressed (1)
Shahidi katika kesi ya  mauaji ya Monica Kimani  alisema kwamba Joseph Irungu maarafu kama Jowie alitambulishwa kwake kama afisa wa polisi wa kimataifa (Interpol) na pia mtaalamu wa masuala ya usalama katika Afisi ya Rais.

Lee Omondi alitoa ushahidi Jumanne kuhusu kesi ya mauaji ya Monica Kimani ambapo Jowie pamoja na mpenziwe wa zamani Jacque Maribe walishtakiwa kwa madai ya mauaji hayo.

Omondi alimwambia Jaji James Wakiaga kwamba alienda nyumbani  kwa Monica Septemba 19,2018 ili kuchukua vyeti vyake na kukutana na Jowie na mtu mwingine aliyemtambulishwa kwa jina la Walid.

Hapo ndipo Maribe alimtambulisha  Omondi kwa Jowie na  Walid. Alimwambia kuwa Jowie ni mtaalamu wa usalama wa Interpool na pia afisa wa usalama katika afisi ya rais.  Walid alitambulishwa kama jirani aliyekuja kumwona  Monica baada ya kutoka Juba ,Sudan Kusini.

Omondi alisema kwamba mtu aliyetambulishwa ni Jowie na alimwona na kumtambua kortini. Jowie ni mshukiwa wa kwanza katika mauaji haya ya Monica.

Omondi alisema walikutana na Monica kule Juba alipokuwa kazini.

Alisema kuwa alipofika, alipewa mvinyo na kukunywa pamoja na Monica na Jowie. Hata hivyo, alisema kwamba kinywaji chake kilikuwa na wiski huku hao wawili wakinywa mvinyo.

Aidha alisema kuwa Jowie alikuwa amevalia kanzu . Monica alimwambia kuwa haikuwa desturi yake kuvali hivyo huku akisema,“Havaangi Kanzu lakini leo amevaa,"

Wakati mmoja tuliongea kuhusu usalama wa nchini Jowie akakubali kunitafutia bunduki wa kila namna na hapo ndipi niliamini kuwa anafanya na idara ya usalama," alisema.

Pia, walizungumzia kuhusu ziara ya Monica ya kwenda Dubai ambapo alisema alifaa kwenda mkutano wa Unicef ulioratibiwa siku iliyofuata.

Alisema kwamba waliendelea kunywa mvinyo kwa muda mrefu huku wakila jikoni.

Korti iliambiwa kuwa Walid alikuwa wa kwanza kuondoka mahali pale.

"Nilikaa kwa muda mrefu kidogo baada ya Walid kuondoka. Baadaye niliwasihi kuondoka na Monica akasema ' Jowie anakufuata sasa,''' Omondo alisema.

Siku iliyofuata, Omondi alisema kwamba hangeweza kuwasiliana na Monica tena. Mwanzo alidhani kuwa alikuwa ameenda ziara yake ya Dubai, ila alifahamishiwa kuwa alikuwa ameuawa.