Mtajiua bure! Hii si dawa ya corona

Tiba
Tiba
Tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha virusi vya Corona nchini  kumekuwa na ushauri  mbali  mbali wa tiba ya virusi hivyo huku watu kadhaa wakijaribu kupendekezwa kutumiwa kwa mchanganyiko wa dawa za miti shamba ,matunda na hata kula vyakula Fulani ili kuzidiaha kinga za miili yao .

Hata  hivyo , baadhi ya ‘tiba’ hizo za kiasili zinahofisha na huenda zikakupa madhara kuliko manufaa .Maajuzi huko pwani kumezuka  ripoti kwamba mtoto  mchanga aliyezaliwa alizungumza na kuwaambia wenyeji kwamba kunywa chai ya mkanda isiokuwa na sukari ikinywea alfajiri ya siku hiyo ndio iliyokuwa tiba ya virusi vya Corona .watu walikimbia kufanya hivyo lakini hadi sasa hakuna ithibati iwapi ‘tiba’ hiyo ilifanya kazi .

Pia watu wengi katika sehemu mbali mbali wamekuwa kichanganya  matawi ya mimea mbali mbali ,ndimu,tangawizi na kadhalika wakidai kwamba mchanganyiko huo uliochemshwa na kutokota unaweza kutibu virusi vya corona.wanasayansi wanasema hawajapta ushahidi kwamba ‘tiba’ kama hizo  zinaweza kutibu  virusi vya corona. Wakati huu ambapo kila anayejali kuanzisha ‘tiba’ yake unashauri kuwa mwangalifu usije ukatumia dawa ambayo hujui madhara yake ni yepi.Kuna waliokimbia katika maduka ya dawa kununua  tembe  na dawa nyingi baada ya uvumi kuzuka mtandaoni kwamba mseto wa dawa mbali mbali za kutibu malaria unaweza kutibu virusi vya Corona .

Unafaa kujua kwamba baadhi ya dawa zinaweza kuwa sumu na kusababisha madhara ya  kiafya au hata kifo endapo yatatumiwa bila ushauri wa daktari.