Mudavadi amepitisha muda wake kama kiongozi wa ANC-Msajili wa vyama

Msajili wa vyama vya kisiasa  Anne nderitu  amesema kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi amezidisha  muda wa hatamu yake  kileleni mwa chama hicho.

Nderitu amekataa kuongeza muda huo wa miaka mitano akingoja marekebisho   yua ombi la chama hivho kutaka muda wa Mudavadi kama kiongozi wa ANC kuzidishwa hadi baada ya janga la Covid 19 .

Katiba ya ANC  maafisa wa chama watachaguliwa kuhudumu kwa miaka mitano  ambapo baada ya muda huo uchaguzi utaandaliwa na maafisa wapya kuchaguliwa .

Mnamo juni  tarehe 26 ANC  iliamua kupitia  mkuano maalum wa baraza la usimamizi  kwamba wale ambao muda wao kuhudumu umekamilika wataendelea kushikilia nafasi hizo hadi baada ya janga la corona .

Hatamu ya washikilizi wa nafasi hizo akiwemo Mudavadi ilitamatika Juni tarehe 15

Katika jaribio la kufuata katiba yake chama hicho kilisongesha mbele uchaguzi wake hadi baada ya janga na corona .Iliwasilisha ombi hilo kwa msajili wa vyama Anne Nderitu  .

Siku ya Jumanne Nderitu ameliambia gazeti la The Star  kwamba  afisi yake imekataa ombi hilo la ANC  kuzidisha muda wa washikilizi wa nafasi za uongozi  kwani pendekezo hilo linazuiwa na mianya na ukiukaji wa sheria inayosimamia vyama vya kisiasa

“ Kuna mianya na msajili wa vyama amekishauri chama cha ANC kurekebisha na kuziba mianya hiyo kwanza ili kuafikiana na mahitajiya sheria ya vyama vya kisiasa’ amesema Nderitu kupitia simu