Mwanaume ajirusha kutoka kwa matatu na kuaga dunia

Polisi huko Voi kaunti ya Taita Taveta wanachunguza kisa ambaccho mwanamume wa umri wa makamo alifariki kwa njia tatanishi baada ya kujirusha kutoka kwa matatu.

Inadaiwa kuwa mwendazake alifariki baada ya kujirusha kupitia kwa dirisha la matatu alimokua akisafiria kutoka mjini Mombasa hadi Voi.
Polisi pia wanafanya uchunguzi kubaini anakotoka mwanamume huyo kwani hakuwa na stakabadhi yoyote ya kumtambulisha.

Kwingineko, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 50 ameaga dunia baada ya kugongwa na gari katika soko la Ochude kwenye barabara ya Busia kuelekea mayoni.

Wananchi wanasema mwanaume huyo alikuwa anatembea kwa miguu kutoka nyumbani kwake Ochude akielekea soko la Kemodo saa nne usiku, wakati aligongwa na kuuawa papo hapo na gari ambalo halijulikani lilitoweka baada ya ajali hiyo.

Mwili wake uliondolewa mahala pa ajali na kupelekwa kwenye chumba cha wafu cha hospitali ya rufaa Busia na maafisa wa polisi wa Busia ambao wameanzisha msako dhidi ya gari hilo.