Mwili Wa Mwanaume Wapatikana Bungoma

Maafisa wa Polisi mjini Bungoma wameanzisha uchunguzi kufuatia kupatikana kwa mwili wa mwanaume mmoja akiwa ameuawa katika eneo la shell viungani mwa mji huo.

Akidhibitisha kisa hicho OCPD wa Bungoma kusini David Kirui amehoji kuwa walipashwa kupatikana kwa mwili huo na mwanamke mmoja mwendo wa asubuhi alipokuwa akipeleka mwanawe shuleni ambapo ulikuwa umelazwa langoni pake ukiwa na majeraha kichwani.

Kiruia amewataka wananchi kupasha maafisa wa usalama visa vyovyote visivyo vya kawaida hasa nyakati za usiku.

Mwili wa mwanaume huyo umehifadhiwa katika hifadhi ya hospitali ya rufaaa ya kaunti ya Bungoma.

-Brian Ojamaa