casket (1)

Mwili wapotea katika chumba cha kuhifadhia mauti Bungoma

Jamii moja iliyopoteza mpendwa wao na wakaazi wa kijiji cha Nakalira eneo bunge la Kimilili kaunti ya Bungoma imeshtuka baada ya kuukosa mwili wa marehemu Mary Nasimiyu  Zacharia mwenye umri wa miaka 74 katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya misheni ya Dreamland kimililili.

Eric Omondi atokwa na povu insta. Afunguka jinsi Ebru ilivyomtesa Chipukeezy

Kulingana na Dr. longinus Wekesa ambaye ni mmoja wa jamii ya marehemu Mary Nasimiyu zacharia amesema kuwa juhudi yao kuuchukua mwili huo hadi nyumbani Nakalira iligonga mwamba walipogundua kuwa mwili ulikuwa umetoweka kwa njia tatanishi.

Walipofuatilia, ilisemekana kwamba mwili wao ulichukuliwa na jamii moja kutoka kijiji cha Mufungu eneo bunge la Sirisia na mazishi ilifanyika siku ya Ijumaa iliyopita bila kufahamu kuwa haukuwa mwili mwao.

Kung’uta miwa! Uganda yaidhinishwa kusafirisha bangi ulaya

Nayo jamii kutoka Sirisia iliyo uchukuwa mwili huo kimakosa ikiongozwa na mtoto wa marehemu wa mwili ulioachwa, Benjamini Simiyu Wekesa, imethibitisha kuwa huenda walizika mwili huo kimakosa akidai kuwa wamethibisha mwili wao ungali katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hispitali hiyo kwa jina Grace Nakhumicha Wekesa.

Naye msimamizi wa hospitali hiyo Bi. Ruth Nabie amesema kuwa kijana wa marehemu kwa jina Eric ndiye aliwaharakisha kuutoa mwili akisema makosa ilikuwa ya jamii ya marehemu Grace Nakhumicha Wekesa.

Inspekta Mwala anusurika kichapo cha umati. Agonga na kuua mtu papo kwa hapo

-Brian Ojamaa

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments