Nairobi Na Mombasa Zimeandikisha Idadi Kubwa Ya Watu Waliolawitiwa

ulawiti
ulawiti

Watu wanaoishi katika kaunti za Nairobi na Mombasa wamo katika hatari kubwa ya kulawitiwa ikilinganishwa na kaunti zingine zote humu nchini.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde ya shirika la Health Care Assistance Kenya.

Kwenye ripoti hiyo kaunti za Nairobi na Mombasa zimeandikisha idadi kubwa ya watu waliolatiwa.

Katika kipindi cha mwezi Juni pekee jumla ya watu 96 Nairobi  waliripotiwa kulawitiwa huku Mombasa ikiandikisha watu 45.

Akizungumza na wanahabari jijini Kisumu, afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo Fanice Lisiagali ameelezea kutamaushwa kwake na dhuluma nyingi za kijinsia akisema hali hii  ambao inatishia kuzima matumaini ya mtoto wa kike kujihusisha na siasa hasaa baada ya baadhi ya wanasiasa wa kike kukabiliwa na baadhi ya dhulma.

Lisiagali ametoa wito kwa  jamii kutangaza dhuluma hizi ili kutoa nafasi kwa haki kuchukua mkondo wake huu wahusika watendwa wa dhulma hizo wakabiliwe kisheria.

-The Star| Musa Naviye