‘Nanenepa tu, sitaki mtoto mwingine.’ Asema mwanamuziki Wahu Kagwi

Wahu  na  Nameless  ni  'macelebs' wenye ndoa inayotamaniwa na  wengi nchini. Wawili hao wamekuwa kielelezo kwa wengi kwani wamestahimili milima na mabonde katika uhusiano wao lakini bado wanaibuka kuwa thabiti.

Wahu na Nameless pia sio watu wa kuigiza kuhusu maisha kwani wao husema ukweli kuhusu ugumu  na changamoto  za ndoa bila kuficha au kupaka rangi mambo katika maisha yao. Wahu ambaye ni  mama ya wasichana wawili warembo, maajuzi  amezungumza kuhusu kupata mtoto mwingine. Katika mahojiano na Word Is,  msanii huyo mwenye umri wa miaka 40  amesema amefunga uzazi.

Namless na Wahu wamekuwa pamoja kwa miaka 15 na yaonekana washafanya uamuzi wa kufunga sura ya uzazi kwani Wahu ana lalama zake akisema;

“ Nazidi kunenepa tu , sifikiri nataka mtoto mwingine. Mtoto huchukua miaka yako mitatu kabla aweze kujifanyia lolote …’

“ Niko sawa. Kifunga mimba wangu Nyakio anakaribia kutimu umri wa miaka saba  na nafurahia kwamba anajifanyia vitu vingi mwenyewe; anaoga  na kula pekee yake …’

Msanii huyo wa gospel  anasema anafahamu kwamba baraka huja kupitia watoto lakini ameridhika na wawili hao. ‘ Ni raha lakini mimi nimeridhika na wasichana wangu wawili.’  Wahu anasema.

Msimamo wake hata hivyo unakinzana na wa mume wake Nameles ambaye miaka michahe iliyopita alifichua matamanio yake ya kupata mtoto mwingine  mvulana... Hadi sasa vitakuwa vita vya panzi na huenda Nameless  akisinzia basi mkewe Wahu atakuwa na usemi wa mwisho na kufunga kabisa  fursa ya yeye kuwa baba ya ‘ndume’.