Nilibakwa na sasa nina hofu mabinti wangu watabakwa pia

Nchi ya Afrika Kusini imekuwa ikikumbwa na majanga mengi ya ubakaji na mauaji ya wanawake wiki chache zilizopita, ikiwemo wasichana wa shule na hata wasichana wengi wa vyuo vikuu waliobakwa na hata kuuwawa.

Mpiga picha mmoja, Sarah Midgley mwenye umri wa miaka 37, alifunguka na kusema kuwa mpaka wa sasa, anajaribu kupona kufikiria yaliyo mpata karibu miaka kumi iliyopita.

Binti huyu alisema kuwa, aliyekuwa mpenzi wake, alikuwa akimbaka na kumtukana kila siku kwa miezi kumi na nane kabla apate ujasiri wa kutoka kwa nyumba hiyo.

Zaidi ya hayo, Midgley alisema kuwa alijaribu sana kutoka kwenye nyumba hiyo lakini kila wakati angejaribu, alishindwa na pia hakuwa na uwezo wa kuwaambia watu wengine kwani aliaibika kutokuwa na uwezo wa kujichunga.

Jamaa huyu alikuwa anampiga mateke na hata wakati mwingine kutishia kumuua, atawabaka watoto wake na kuwaua mbele ya macho yake.

Vilevile, alikuwa ametengwa na watu wote mjini kwani alikuwa amepewa talaka na mpenzi wake akawa amemesisitizia kuwa, wazazi na marafiki wake hawakuwa wanamjali.

Binti huyu alipopata ujasiri wa kutoka kwenye nyumba hii alitoka lakini siku kumi baaadaye, mpenzi huyo akampata bado na kumwomba lifti mpaka alipokuwa akienda akidai kuwa, hana nauli.

Midgley kwa uzuri wake, alimpa lifti lakini akaja kujuta baadae. Aisee majuto ni mjukuu.

Baada ya Jamaa huyu kupewa lifti na kufika walipokuwa wakienda, alimgeukia Midgley na kumbaka na alipomaliza, rafiki yake pia akaendelea. Ama kwa hakika, kuna watu wasio na utu.

Midgley aliokolewa na binti flani aliyekuwa kwenye mtaa huo na kuita ambulensi papo hapo. Midgley alipelekwa hospitalini na kupewa matibabu.

Baada ya muda usiokuwa mrefu, alipata ujumbe kuwa jamaaa huyu alikuwa amekamatwa na kufungwa jela, na hapo ndipo alijaribu kuishi kwa amani kidogo.

Hata hivyo, mama huyu mwenye mabinti wawili anaogopa kuwa kitendo hicho kinaweza kuwafanyikia watoto wake na kwa hivyo, amejaribu juu chini kuwalinda mabinti wake na mara kwa mara kuwaambia kuwa wanaweza kumwambia kitu chochote.

Maanake, wasiogope kusema endapo mambo hayaendi yanavyo faa kuenda.

-BBC