Njoo Jubilee Kalonzo tusaidie kujenga Kenya, asema Ruto

Kalonzo-Ruto
Kalonzo-Ruto
Naibu wa rais William Samoei Ruto amemkaribisha kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka katika chama cha Jubilee.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Ruto ametangaza kuwa kiongozi huyo asiwe na wasiwasi wowote kujiunga na chama tawala.

"Karibu Jubilee Stevo tusaidie kujenga, chama chenye maono na cha watu wote," alisema Ruto .

Tamko la Ruto linajiri siku chache baada ya kudharaulia mbali mashtaka ya gavana wa Machakos Alfred Mutua kuwa anapanga njama ya kumuua.

Mutua aliandikisha taarifa katika kituo cha polisi kuwashtaki Ruto, Duale na Murkomen .

"Nilishambuliwa na mheshimiwa Duale na Murkomen kwa kuniambia ya kwamba ninawashambulia. Nilipowauliza eti ninawashambulia vipi wakasema eti nimekuwa nikimshambulia Ruto," Mutua amesema.

Kinara huyu wa chama cha Wiper yupo katika wakati mgumu baada ya magavana wake kuonyesha ubabe wa kisiasa katika uchaguzi mdogo Kibra.

Aidha, siku chache nyuma, aliyekuwa seneta wa Machakos Muthama alitaja uwezekano wa Kalonzo kuunda muungano wa kisiasa na William Ruto.

"Hivi karibuni nitawaleta pamoja viongozi wote kutoka eneo hilo kuanzia wabunge na MCAs ili kujadili mwelekeo huo. Urafiki wetu kisiasa na kinara wa ODM Raila Odinga uliisha. Tutafanya mazungumzo na Ruto, Musalia na Moses Wetangula," alisema Muthama.

Kalonzo alikataa taarifa hizi.