PATANISHO:Nampenda sana mke wangu wa pili kuliko wa kwanza-Fredrick Ochieng

Katika PATANISHO kipindi leo Gidi na Ghost, walijizatiti kumpatanisha Fredrick Ochieng,28, na mamake mkwe Dorfin.
"Nikosana na mama mkwe na baada ya siku chache alimtuma nduguye mkew wangu kumchukuwa na nguo zake kumpeleka kwao," Alieleza Ochieng.

Ochieng alieleza zaidi na kusema kuwa alikuwa na mke wa kwanza lakini alikua msumbufu sana kuliko wa pili.

"Mke wangu wa kwanza alirudi lakini simpendi na mpenda mke wa pili na hasumbui kama yule wa kwanza.

"Nilimjua mke wangu wa pili kwa mwaka mmoja na nusu," Alisema Ochieng.

Mama mkwe aliopigiwa simu alimpokeza simu mke wa Ochieng na kusema kwamba mamake ndiyo kikwazo lakini atatoroka kwa maana pia naye anampenda sana Ochieng.

"Mama ndiyo ako na shida lakini nitatoroka nirudi  kwa mume wangu," Alisema Cynthia.

Bwana Ochieng alikiri kuwa anampenda sana Cynthia kwa sababu alimlinda vyema walipokuwa pamoja.

Cynthia alisema pia atarudi kwa mumewe Ochieng katika muda mfupi ujao.

Ochieng aliendelea kusema kuwa atamjengea mke wake wa pili nyumba ili wasiweze kuzozana na mke wake wa kwanza.

"Nitamjengea nyumba aishi ili wasizozane na mke menza, mke wangu wa kwanza ana shida zake lakini Cynthia hana shida yeyote," Ochieng Alisimulia.