PATANISHO: Bwanangu aligeuka kuwa deadbeat

Jennifer alituma ujumbe akiomba apatanishwe na bwanake Abraham ambaye walikosana mwaka wa 2016.

Kukosana naye sielewi kwani wakati huo nilikuwa mja mzito na labda nilikuwa na hasira. Isitoshe alikuwa anaingia nyumbani akiwa amechelewa na majukumu yake yakashuka, hakuwa analipa rent wala school fees.

Sasa nikamuuliza kwani ana familia nyingine akadai manyumba ni mengi na akaondoka. Sasa nilipojifungua alinitoa hospitalini na tukaagana aniletee vitu vya mtoto lakini sikumuona.

Siku moja akarudi na kupanga nguo zake na kuondoka." Alieleza Jennifer akidai kuwa alikuja kugundua mumewe anaishi na mwanamke mwingine aliye na watoto watatu.

Wawili hao wameishi kwa ndoa ya miaka kumi na miwili na wana watoto watatu.

Baada ya kupigiwa simu, bwana Abraham alikataa kuzungumza nasi.

&feature=youtu.be