PATANISHO: Hasira zilifanya nimpige babangu wa miaka 60

Bwana Tobias aliomba apatanishwe na babake mzazi akidai kuwa mwaka wa 2017 alimpiga babake baada yake kumtwanga na fimbo kwa kukosa kumaliza shughuli ya ukulima.

"Wakati nilikuwa napanga makaa nikaona baba akija na fimbo na alipofika nikamtwanga mara tatu nikamwangusha chini na nikatoweka mbio kwani sikutaka nimpige. Tangia hiyo siku huwa tunazungumza naye lakini najua hajanisamehe." Alieleza Tobias.

Alipopigiwa simu babake Tobias alimuamrisha mwanawe amtumie elfu mbili.

"Sasa fanya hivi, nitumie elfu mbili kwani ilikuwa makosa." Alisema.

Nimemsamehea lakini anitumie shilingi mia tano nimepunguza kwa ajili ni damu yangu, ama aninunulie blanketi." Alisisitiza.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be