PATANISHO: Juma Na Akinyi Washindwa Kupatana

Siku ya Jumatatu, 19/9/2016 Juma alituma arafa apatanishwe na mkewe Akinyi baada ya wawili hao kukosana akidai huenda wawili hao wangetekeleza mambo mabaya.

Huku wakijaribu kunasua ndoa yao, Gidi na Ghost hawakujua lilokuwa mbele yao kwani patanisho iligeuka kuwa mashindano ya kukemeana na kelele tupu hewani.

Kulingana na Akinyi ambaye aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu, walikosana na Juma wakiwa mjini Nakuru huku bwanake akimshuku kuwa ana mipango ya kando na kuelekea Nairobi, huku akiwaacha wanao watatu.

Huku akijieleza, Juma alifichua kuwa baada ya kuwasili Nairobi alioa mke wa pili ili kupunguza hasira bila kujua kuwa alikuwa mke wa wenyewe ambao wamebarikiwa na watoto pamoja.

Lakini wakti wawili hao walipewa fursa wasameheane, hapo ndipo moto uliwaka na wakafokiana bila suluhisho lolote. Do! skiza kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be