PATANISHO: Mimi Na Bwanangu Tulikosania Tu Shilingi Mia Mbili

Bi Patricia alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe Douglas ambaye walikosania shilingi mia mbili.

"Nilikuwa mgonjwa sasa akaniitia daktari kwa nyumba na daktari akamueleza kama ana mia mbili ampatie na bwanangu akafanya vile. Sasa wiki mbili zilipopita sikujua hizo fedha zilikuwa deni.

Sasa akaniitisha mia mbili nikamuuliza gani akadai kuwa zile fedha alipatia daktari anazitaka. Huyu ni bwana tumeoana kwa miaka minne na tumejaliwa mtoto mmoja.

Isitoshe mimi ndiye nanunua kila kitu kwa nyumba licha yake kuwa na kazi nzuri." Alieleza Patricia.

Kulingana na bwana Douglas, "Huyo nimemmiss lakini kuna vile alinikosea tukajaribu kuongea lakini akawa mkali nikajaribu kumfuata lakini huenda marafiki zake wanampotosha."

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be