PATANISHO: Mimi sio mke wako! Aliyekuwa bibi yako aliolewa

Jonathan shabiki wa radio Jambo, aliomba apatanishwe na aliyekuwa mkewe, bi Florence Mueni, ambaye cha kushangaza ni kuwa wawili hao walitengana mwaka wa 2016.

"Tangia tuwachane tumekuwa tukiwasiliana lakini huwa ananiambia kuwa atarudi lakini hajawahi rudi." Alisema Jonathan.

Nilielekea kazini siku moja na niliporudi sikumpata kwani alikuwa amebeba karibu kila kitu kwa nyumba. Aliondoka bila mimi kumkosea na isitoshe naskia alipata mume mwingine." Aliongeza akisema alikuwa anampenda sana.

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja ambaye aliondoka na Mueni baada ya ndoa ya miaka minane.

Alipopigiwa simu, Mwanadada aliyejibu simu alidai kuwa yeye sio mkewe Jonathan na kuwa amekuwa akimpigia simu mara kadhaa. Isitoshe anamjua Mueni kwani aliwahi muomba simu siku moja.

"Huyu hushinda akinipigia simu akidai mimi ni mkewe na nimeishi nikimwambia mimi sio Mueni. Mueni aliwahi niomba simu ampigie lakini sasa ameolewa kwa hivyo Jonathan awache kunisumbua." Alisema bi Agnes.

Yeye hunitumia ujumbe akisema 'sasa my dear umenitupa' imagine na nina bwana. Aendelee na hizo mipango zake za kando zenye zilifanya awachwe." Aliongeza akimkanya Jonathan kuhusu maneno hayo.

Akijitetea, Jonathan alikana kuwa hajawahi kuwa na mipango ya kando.