pata patanisho

PATANISHO: Mke wangu ameavya mimba mbili akiogopa kufutwa kazi na muhindi

Ochieng alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Grace, waliyekosana mwaka uliopita mwezi wa kumi na moja.

“Kuna kazi nilisafiri kidogo na wakati nilirudi kuna msichana alikuwa rafiki yangu ambaye tulipata njiani na bahati mbaya mke wangu alikuwa hapo karibu.

Sasa kwenda nyumbani tukagombana kidogo na nilipotoka kwenda nyumbani nilipata ameondoka na kwenda kwa shangazi yake.” Alijieleza Ochieng.

PATANISHO: Nilimpiga mke wangu hadi nikamvunja mkono

Wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka minne na bado hawajajaliwa watoto.

Ochieng alieleza mbona wawili hao bado hawana watoto na sababu yake iliwashtua wengi.

Amekuwa na tabia ya kuavya mimba kila mara anashika mimba.

Kuna siku alikuja kwa nyumba akanidanganya kuwa alianguka na akaanza kuzoa damu. Kumpeleka hospitalini daktari aliniambia kuwa alikuwa anajaribu kuavya mimba na mtoto akafariki.

Isitoshe kuna siku yeye mwenyewe akiniambia kuwa aliavya mimba eti anaogopa kuwa atafutwa kazi na muhindi aliyemuajiri.

PATANISHO: Sitasema kama namtambua Beryl kama mke wangu

Babangu alipumzika wiki iliyopita na twapaswa kumzika wiki ya tarehe ishirini na tatu na kulingana na wazazi hatuwezi fanya mazishi kama mke wangu hayuko kwa boma.

Wakati tulizungumza alisema atakuja lakini bado hajaja, jana nilimpigia lakini aliruka hayo yote.

Hata hivyo, juhudi zetu za kumfikia bi Grace hazikufua dafu.

PATANISHO: Nahisi kujitia kitanzi kwa sababu ya mume wangu

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments